WANANCHI wanaopata huduma ya umeme unaotokana na gredi ya Taifa ni asilimia 11 pekee ambapo asilimia moja ya wananchi waishio vijijini, ndio wanaonufaika na umeme huo.
Hali hiyo inachangia kukwamisha huduma mbalimbali za kijamii hususani katika maeneo ya vijijini ambayo yanahitaji nishati hiyo ili kuboresha mahitaji mbalimbali yakiwemo huduma bora ya afya kwa watoto na wakinamama wajawazito wakati wa kujifungua.